9 Juni 2015 - 12:05
Mazungumzo ya kutafuta amani nchini Libya yaendelea Morocco

Jumuiya ya kimataifa imeimarisha jitihada zake, ilikupata suluhisho la mgogoro wa Libya. Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa anayehuswika na Libya Bernardino Leon na wawakilishi wa serikali mbili zinazokinzana nchini humo wamewasilisha pendekezo la kufikia makubaliano kufuatia mazungumzo katika mji wa mwambao wa Skhirat nchini Morocco.

Kwa mujibu wa Shirika la habari la Ufaransa AFP, wawawikilishi wa pande zote mbili  wanakwenda Berlin leo kwa mazungumzo zaidi. Mazungumzo yao yamepangwa kuwa pamoja na  wajumbe wa ngazi ya juu wa  kundi la nchi 7 zilizoendelea kiviwanda –G7.

Mwakilishi wa Uhispania katika Umoja wa Mataifa amezitaka pande zote mbili katika mgogoro huo wa Libya kuwasilisha pendekezo hilo  kwenye mabunge yao na baadae wakutane tena nchini morocco wiki ijayo. Tangu alipopinduliwa Muammar Gadaafi 2011, Libya imekubwa na machafuiko.  Katikati ya mwaka jana  wanamgambo wa kundi la kigaidi la Daesh waliuteka mji mkuu Tripoli na kuunda serikali yao wenyewe ambayo haitambuliwa na jumuiya ya kimataifa. Serikali inayotambuliwa imekimbilia mji wa mashariki wa Tobruk pamoja na bunge lake.